Wananchi wa Jordan leo wameelekea kwenye vituo vya
kupigia kura kuwachagua wabunge baada ya mabadiliko ya sheria za uchaguzi
yaliyokishawishi chama cha upinzani cha Islamic Action Front (IAF)kurudi kwenye
jukwaa la kisiasa baada ya kupita muongo mmoja.
Mchakato wa upigaji kura ulianza leo asubuhi na
unatarajiwa kudumu kwa muda wa saa 12.
Zaidi ya wapiga kura milioni 4 wenye umri wa miaka 17
wanatarajiwa kuwachagua wabunge 130 kati ya wagombea 1,252 watakaohudumu kwa
muhula wa miaka 4.
Miongoni mwa viti hivyo, viti 15 vimetengwa kwa ajili ya
wanawake, 8 kwa ajili ya Wakristo na 3 kwa ajili ya wawakilisha wa Wachechenia
na Circassia ambao wanaunda jamii za watu wachache nchini humo.
Kwa mujibu wa tume ya uchaguzi nchini humo, waangalizi
wa ndani wapatao 14,000 na wengine 676 kutoka nje ya nchi wanafuatilia uchaguzi
huo. Miongoni mwa waangalizi hao, waangalizi 66 ni kutoka Jumuiya ya Umoja wa
Ulaya.
Hayo yanatokea wakati ambapo chama cha Islamic Action
Front (IAF)--- chama cha upinzani chenye nguvu – ambacho kiligomea chaguzi
mbili zilizopita, kilitangaza mwezi Juni kuwa kingeshiriki uchaguzi huo baada ya
sheria ya uchaguzi kufanyiwa ya mabadiliko.
Chama cha IAF, ambalo ni tawi la kisiasa la vuguvugu la
Udugu wa Kiislamu (Muslim Brotherhood), kilishiriki katika uchaguzi wa bunge wa
mwaka 2007, lakini kiligomea chaguzi za mwaka 2010 na 2013 kikipinga mfumo wa
uchaguzi na tuhuma za wizi wa kura.
Msemaji wa chama hicho, Murad Adayleh, ambaye pia ni
miongoni mwa wagombea, amesema kuwa chama chake kitasukuma agenda ya mabadiliko
ya kiuchumi na kielimu katika harakati za “kufichua sera mbovu za serikali na
kuweka wazi makosa yote ya sera hizo”.
Alisema kuwa chama chake kinatarajia kushinda kuanzia
robo moja mpaka theluthi moja ya viti 130 vya ubunge.
Sheria moya za uchaguzi unaviruhusu vyama kuwa na orodha
kubwa, badala ya mfumo wa “kura moja” ambao uliwanufaisha wagombea wa makabila,
kwa mujibu wa serikali. Walibadilisha mfumo wa “mtu mmoja, kura moja” ambao
uliwekwa mwaka 1993 na kuvidhoofisha vyama vya kisiasa.
Hata hivyo, wakosoaji wanasema kuwa mabadiliko ya mfumo
huo bado yanaendelea kuwanufaisha na kuwapendelea wafuasi wa kikabila wa Mfalme
Abdullah II wa nchi hiyo. Wanasema kuwa bunge jipya litakuwa sawa na bunge
linalomaliza muda wake, ambalo lilikosolewa na wananchi kwa kushindwa
kushughulika tatizo la ukosefu wa ajira na matatizo mengine.
Mapema mwaka 2015, bunge lilipitisha mabadiliko ya
kikatiba yaliyompa mfalme haki ya moja kwa moja kuwaajiri na kuwafukuza wakuu wa
jeshi, wakuu wa idara za usalama, majaji
na wabunge wa bunge la seneti bila ithibati ya serikali.
Kabla ya hapo, haki pekee ya mfalme Abdullah II ilikuwa
ni kumteua moja kwa moja waziri mkuu.
0 comments:
Post a Comment