Mwanamke akiwa amebeba dumu katika kambi ya wakimbizi wa ndani iliyowekwa katika Kaga Bandoro kaskazini mwa mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Oktoba 19, 2016. |
Kwa uchache watu 16 wamepoteza maisha na maelfu ya raia
kuyakimbia makazi yao katika Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati wa makabiliano
kati ya makundi mawili ya waasi yanayohasimiana nchini humo, Umoja wa Mataifa
umesema.
Umoja wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA, umetoa
tangazo hilo na kuongeza kuwa awamu hiyo mpya ya ghasia ililipuka siku mbili
zilizopita kati ya pande mbili hasimu ndani ya kundi la waasi wa Seleka katika
mji wa Bria, kiasi cha kilometa 400 kaskazini mashariki mwa mji mkuu, Bangui.
Pande hizo mbili zilipambana katika kugombea udhibiti wa
ushuru kutokakwa kabila la wafugaji la Fulani linalohamahama.
Mwezi Machi 2013, Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia
katika machafuko baada ya rais wa wakati huo Francois Bozize kuondolewa
madarakani na muungano wa waasi wa Seleka na hatamu za madaraka kushikiliwa na Michel
Am-Nondokro Djotodia, Muislamu wa kwanza kuwa rais katika taifa hilo lenye
Wakristo wengi.
Hata hivyo, mapinduzi hayo yalichochea mfululizo wa
mshambulizi ya kulipiza kisasi kati ya waasi wa Seleka na waasi wa Kikristo
lililojulikana kama anti-balaka, ambao walifanya mashambulizi makubwa dhidi ya
Waislamu wachache nchini humo.
Mtu mmoja kati ya watu 10 wa nchi hiyo yenye raia milioni
4.5 alilazimishwa kukimbiliakwenye maeneo yenye usalama baada ya taifa hilo
kutumbukia katika ghasia za kikabila na kidini. Maelfu ya watu waliyakimbia
makazi yao katika taifa hilo lenye utajiri wa maliasili.
Mwaka 2014, kiasi cha walinda amani 11,000 walitumwa na
Umoja wa Mataifa nchini humo kama sehemu ya kikosi cha MINUSCA.
Mnamo Julai 23, 2014, wawakilishi wa makundi ya Seleka na
anti-balaka walisaini makubaliano ya kusitisha mapigano katika mji mkuu wa
Congo, Brazzaville, lakini nchi hiyo bado haijajikwamua kikamilifu kutoka kwenye
athari za ghasia hizo.
Kupata
habari kwa njia ya WhatsApp wasiliana nasi kupitia: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment