UBALOZI WA MAREKANI UTURUKI WASHAMBULIWA

السفارة الأميركية في أنقرة
Ubalozi wa Marekani mjini Ankara





Ubalozi wa Marekani katika mji mkuu wa Uturuki, Ankara, umeshambuliwa kwa risasi asubuhi ya leo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, mtu mmoja aliyekuwa kwenye gari alifyatua risasi kadhaa kuelekea jengo hilo na kuvunja vioo vya madirisha. Hata hivyo, hakuna majeruhi wala vifo.

Mpaka sasa haijajulikana sababu na chanzo cha tukio hilo, wala mtekelezaji hajatambulika.

Hayo yanajiri katika wakati ambapo Uturuki na Marekani ziko katika mgogoro wa kisiasa na kiuchumi baada ya Washington kuiwekea vikwazo Uturuki kwa madai ya hatua ya Ankara kumshikilia mchungaji Andrew Brunson, ambaye Uturuki inamtuhumu kushiriki katika njama ya mapinduzi yaliyofeli ya mwaka 2016.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment