BURUNDI YAITUHUMU UN KUPIKA TAKWIMU ZA WAKIMBIZI

Warundi waliokimbia ghasia za baada ya uchaguzi wakiwa wamepumzika kandoni mwa Tanganyika huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo baada ya safari ya saa 22 kwa boti. 


Mapema siku ya Jumatano Burundi ililituhumu Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi kuwa “linapika kwa makusudi takwimu za wakimbizi wa Burundi”.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani wa nchi hiyo, Terence Ntahiraja, alisema kuwa UNHCR inakataa kukikiri na kutambua kuwa baadhi ya Wakimbizi wa Burundi wamerejea nchini mwao na kwamba inatumia namba bandia kutafuta misaada.

Bwana Ntahiraja alikuwa akijibu madai yaliyotolewa na UNHCR siku ya Jumanne wakati ikiomba msaada wa dola milioni 391 za kuhudumia wakimbizi wapatao 430,000 kutoka Burundi walioko katika nchi za Tanzania, Rwanda, Jamhuri ya Kidemkorasia ya Kongo na Uganda.

Ntahiraja alisema kuwa UNHCR inadai wakimbizi hao 430,000 walikimbia tangu mwaka 2015 na wanaishi katika makambi ya wakimbizi. Aliendelea kusema kuwa idadi hiyo sio sahihi kwa sababu zaidi ya wakimbizi 200,000 wamesharejea nchini Burundi.

Kwa mujibu wa mpango wa mwaka 2018 wa kuisaidia Burundi, UNHCR inadai kuwa hali ya Burundi inaonekana kuwa ya kutisha na kwamba wanapata asilimia 21 tu ya fedha zinaazohitajika.

Tangu mwaka 2015, zaidi ya wakimbizi 400,000 na watafuta hifadhi waliikimbia Burundi wakikwepa ukiukwaji wa haki za binadamu, ukosefu wa uthabiti wa kisiasa na mzozo wa kibinadamu, ilisema taarifa hiyo ya UNHCR.

Taarifa hiyo pia inaelezea kuwa kiasi cha wakimbizi 50,000 wanatarajia kuikimbia nchi yao mwaka huu.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment