Msemaji wa Ikulu ya Palestina, Nabil Abu Rudeineh |
JERUSALEM
Jerusalem is “haiuzwi”, Maafisa wa Kipalestina wamesema
wamesema leo Jumatano baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutishia kuikatia
misaada ya kifedha serikali ya Mamlaka ya Palestina iwapo haitaanza mazungumzo na
utawala wa Israel.
“Jerusalem haiuzwi, si kwa dhahabu wala fedha,” msemaji
wa Rais wa Palestina, Nabil Abu Rudeineh amesema katika taarifa iliyorushwa na
shirika rasmi la habari la Palestina, WAFA.
“Kama Marekani ina wasiwasi na maslahi yake katika eneo
la Mashariki ya Kati, inapaswa kufungamana na misingi na rejea za Baraza la
Usalama na Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa,” amsema Abu Rudeineh.
“Vinginevyo, Marekani itaishia kulitumbukiza eneo hili
shimoni,” aliongeza.
Abu Rudeineh amesema kuwa uongozi wa Palestina haupingi
kurudi kwenye meza ya mazungumzo, bali “mazungumzo ya kweli yanatakiwa kuwa na
uhalali wa kimataifa na mpango wa amani wa jumuiya ya Kiarabu [mpango wa mwaka 2002
unaoungwa mkono na Saudi Arabia], ambao unatoa wito wa kuundwa kwa taifa huru
la Palestina huku mji mkuu wake ukiwa Jerusalem Mashariki."
Naye msemaji wa vuguvugu la Hamas, Fawzi Barhoum, amekielezea
kitisho cha Trump kama "kitisho rahisi cha kisiasa."
"Vitisho hivi vinaakisi tabia ya kinyama na utovu
wa maadili wa Marekani katika kuamiliana na madai ya Palestina na Wapalestina,"
amesema Barhoum katika taarifa yake mapema leo Jumatano.
“Ili kukabiliana na shinikizo hili la Marekani
kunahitajika juhudi kubwa zaidi ili kufanikisha umoja wa Wapalestina,” aliongeza.
Msemaji huyo wa Hamas aliendelea kusisitiza hitajio la
kuiunganisha “misimamo ya Waarabu, Waislamu na Jumuiya ya Kimataifa katika
kuunga mkono haki za Wapalestina dhidi ya matendo ya Marekani na utawala wa
Wazayuni wa Israel."
Hanan Ashrawi, mwanazuoni wa Kipalestina na mjumbe wa
Kamati Tendaji ya Chama cha Ukombozi wa Palestina (PLO), kwa upande wake
alisisitiza msimamo kwamba haki za Wapalestina “haziuzwi”.
“Kwa kitendo cha kuutambua mji wa Jerusalem unaokaliwa
kimabavu kama mji mkuu wa Israel, sio tu kwamba Trump amekwenda kinyume na
sheria ya kimataifa, bali pia amevuruga mchakato wa amani huku akichochea
vitendo haramu vya utawala wa Israel kuumega mji wetu mkuu,” Ashrawi amesema
katika taarifa yake.
“Hatutatishika,” alisema. “Trump amehujumu amani, haki
na uhuru ambao tumekuwa tukiutafuta na sasa anatutisha kutuadhibu kwa matokeo
ya sera yake iliyokosa akili."
Mnamo Desemba 6, Trump alitangaza uamuzi wake wa
kuutambua mji wa Jerusalem kama mji mkuu wa utawala wa Israel, hatua
iliyosababisha maandamano makubwa na lawama kutoka ulimwengu wa Kiarabu na
Kiislamu.
Tangu wakati huo, kwa uchache Wapalestina 15 wameuawa –
na maelfu kujeruhiwa – katika makabiliano makali na vikosi vya utawala wa
Israel.
Mapema siku ya Jumanne, rais wa Marekani alitishia
kukata msaada wa kifedha kwa serikali la Mamlaka ya Palestina yenye makao yake
mjini Ramallah.
"Tunawalipa Wapalestina maelfu kwa mamilioni ya
dola kila mwaka na badala yake hawatushukuru au kutuheshimu," aliandika Trump
kwenye mtandao wa twitter.
"Hawataki hata kufanya mazungumzo kuhusu amani ya
kudumu na Israel,” alisema. “Tumeitwaa Jerusalem, nje ya meza ya mazungumzo, kipengele
ambacho kilikuwa kigumu zaidi katika mazungumzo, lakini Israel, kwa hilo,
ingelipa gharama kubwa.”
“Kwa kuwa Wapalestina hawataki tena kuzungumzia amani,
kwa nini tuendelee kuwalipa mapesa mengi kiasi hiki? " alihoji.
Awamu ya mwisho ya mazungumzo ya amani kati ya Israel na
Palestina ilivunjika mwaka 2014 baada ya Israel kukataa kuliachia huru kundi la
wafungwa wa Kipalestina licha ya kutoa ahadi hiyo mapema.
Mji wa Jerusalem umeendelea kuwa kitovu cha mgogoro wa
Mashariki ya Kati, huku Wapalestina
wakitumai kwamba Jerusalem ya Mashariki—inayokaliwa kimabavu na Israel tangu
mwaka 1967 – itakuwa mji mkuu wa taifa huru la Palestina.
0 comments:
Post a Comment