Taarifa kutoka mjini Istanbul zinasema kuwa Waafrika
wanne raia wa Liberia wamepigwa risasi na kijana mmoja wa Kituruki
anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20.
Tukio hilo limetokea katika eneo la Mecidiyekoy mjini
Istanbul. Maelezo ya kina juu ya tukio hilo bado hayajatolewa, ila taarifa
zilizoifikia meza ya Mzizima 24 kutoka huko zinaelezwa kuwa chanzo chake ni
ubaguzi wa rangi.
Taarifa hizo za awali zinadai kuwa Waafrika hao walikuwa
katika jengo la Trump tower wakinywa kahawa ndipo kijana huyo wa Kituruki alipoingia,
akachomoa bastola yake akasema: “Siwapendi watu weusi” na hapo hapo
akawafyatulia risasi kadhaa miguuni na kuwajeruhi vibaya sana.
Kwa sasa waathirika hao wanapata matibabu katika
hospitali ya Sisli mjini humo. Inasemekana kuwa tukio kama hilo lilitokea
katika eneo la Kurtulus, Istanbul siku kadhaa zilizopita ambapo kijana mmoja
kutoka Nigeria alipigwa risasi mguuni na kujeruhiwa vibaya sana, hali
inayoonekana kuwa Waafrika wanaonekana kulengwa na baadhi ya magenge ya vijana
mjini humo.
Mzizima 24 inafanya juhudi za kuwasiliana na JUMUIYA YA
WANAFUNZI WA KIAFRIKA NCHINI UTURUKI (TASU) ili kupata maelezo zaidi juu ya
matukio hayo.
0 comments:
Post a Comment