Aprili 6, 1994 ni siku ya masaibu kwa Rwanda. Ni siku
ambayo ndege ya rais ilitunguliwa kwenye uwanja wa ndege wa Kigali na kumuua
aliyekuwa rais wa nchi hiyo Juvenal Habyarimana na mwenzake wa Burundi Cyprien
Ntaryamira pamoja na watu wengine 14.
Siku iliyofuata, mauaji ya halaika yalianza nchini humo.
Hivyo, kifo cha Habyarimana kilichochea moto wa mauaji ya watu wapatao milioni
moja ndani ya siku 100. Wahanga wakubwa walikuwa Watutsi na Wahutu wenye
msimamo wa wastani.
Hata hivyo, inaonesha kuwa mbegu ya mauaji ya kimbari
ilikuwa imepandwa miaka mingi kabla, na matokeo yalianza kuonekana wakati wa
maasi ya mwaka 1959 ambapo inaelezwa kuwa zaidi ya watu 20,000 waliuawa.
Pamoja na hayo yote, swali la:
“Ni nani aliyeitungua ndege ya Rais Habyarimana?” bado
halijapata jibu muafaka na lisilokuwa na shaka.
Ni dhahiri kuwa mauaji hayo ya kimbari yataendelea kuwa
doa kwa bara la Afrika na dunia kwa ujumla, na yumkini maswali mengi yenye
utata yasipatiwe majawabu mujarabu.
0 comments:
Post a Comment