UMOJA WA MATAIFA UNAONA FEDHEHA KWA YALIYOTOKEA RWANDA

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa Umoja huo bado unaona fedheha kwa kushindwa kuzuia mauaji ya kimbari yaliyotokea mwaka 1994 nchini Rwanda.

Hayo ameyasema wakati akiwahutubia maelfu ya watu mjini Kigali wakati nchi hiyo ikianza wiki ya maadhimisho ya 20 ya mauaji hayo yaliyoshuhudia watu wapatao milioni moja wakiuawa ndani ya siku 100.

Wakati wa maadhimisho hayo watu wengi walizidiwa kwa hisia na uchungu, huku wengine wakizimia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment