Thibaut Courtois |
Klabu ya Chelsea
huenda itafaidika na kiasi cha paundi milioni 6, endapo itapangwa na klabu ya
Atletico Madrid katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa
barani Ulaya.
Chelsea
wanajipanga kupokea kitita hicho cha pesa, kama wataangukia mkononi mwa Atletico
Madrid katika hatua hiyo kufuatia kifungu kilichopo kwenye makubaliano ya klabu
hizo mbili wakati The blues wakikubali kumpeleka kwa mkopo mlinda mlango kutoka
nchini Ubelgiji Thibaut Courtois huko Estadio Vicente Calderón.
Imeripotiwa
kwamba katika makubaliano hayo, kuna kifungu ambacho kipo kwenye mkataba wa
mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 21 ambacho kinaishurutisha klabu ya
Atletico Madrid kutomtumia Thibaut Courtois endapo itatokea wanakutana na
Chelsea kwenye michuano ya kimataifa.
Kifungu hicho
kimeendelea kusisitiza kwamba endapo Atletico itawalazimu kumtumia kipa huyo
itawagharimu kuwalipa Chelsea kiasi cha paund million tatu kwa kila mchezo
watakaomtumia Thibaut Courtois.
Kama klabu hizo
zitapangwa kukutana katika mchezo wa hatua ya nusu fainali, na Atletico Madrid
wakafanya maamuzi ya kumchezesha mlinda mlango huyo katika mchezo wa nyumbani
na ugenini, itawalazimu kuwalipa Chelsea paund million 6.
Hata hivyo
kitendawili cha Atletico Madrid kupangwa na Chelsea katika mchezo wa hatua ya
nusu fainali, kitateguliwa kesho mara baada ya upangaji wa michezo ya hatua ya
nusu fainali, ambapo hafla yake itafanyika mijini Nyon nchini Uswiz.
Atletico Madrid
wamefanikiwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya
mabingwa barani Ulaya, baada ya kuifunga FC Barcelona bao moja kwa sifuri
katika mchezo uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo huko jijini Madrid.
Baada ya ushindi
huo klabu hiyo Estadio Vicente Calderón, imesonga mbele kwa jumla ya mabao
mawili kwa moja na kuungana na FC Bayern Munich, Chelsea pamoja na Real Madrid
ambazo zimetinga kwenye hatua ya nusu fainali.
0 comments:
Post a Comment