Meneja wa klabu ya Man Utd David Moyes, amesema makosa ya
kipuuzi yaliyofanywa na wachezaji wake wakati wa mchezo wa dhidi ya FC Bayern
Munich yaliwagharimu na kujikuta wakikubali kufungwa mabao matatu kwa moja.
David Moyes, ametupa lawama hizo kwa wachezaji wake kwa
kigezo cha mabao yaliyofungwa na wapinzani wao ambayo yalionekana kuwa mepesi
zaidi ya bao lililotangulia kufungwa na beki wa pembeni wa Man Utd Patrice
Evra.
Moyes, amesema kukosekana kwa umakini kulichangia kwa kiasi
kikubwa kwa Man utd kutupwa nje ya michuano hiyo, hali ambayo amekiri
haikumpendeza, kutokana na mchezo ulivyokua, ambapo ilionekana walikua na
nafasi nzuri ya kupata ushindi katika uwanja wa ugenini.
Meneja huyo kutoka nchini Scotland amesema kulikua hakuna
sababu kwa wachzaji wake kubweteka, baada ya kuongoza kwa bao moja lakini
matokeo ya udhaifu huo yalinekana sekunde kadhaa kutokana na FC Bayerrn Munich
kupata bao la kusawazisha lililofungwa na mshambuliaji kutoka nchini Croatia Mario
Mandzukic, ambae aliumalizia kwa kichwa mpira uliokuwa umepigwa na mshambuliaji
wa pembani kutoka nchini Ufaransa Franck Ribery.
Hata hivyo David Moyes hakuishia hapo katika hatua ya
kuchambua makosa yaliyofanywa na wachezaji wake, hususana wa safu ya ulinzi
ambao bado waliendelea kuoonyesha umakini kwa kushindwa kuzuia ipasavyo mpira
uliokuwa umepigwa kutoka pembeni na Arjen Robben kabla ya Thomas Muller kufunga
kwa urahisi tena akiwa kati kati ya mabeki wa mashetani wekundu.
Kwa upande wa bao la tatu, Moyes ameendelea kuilaumu safu
yake ya ulinzi kutokana na kitendo cha kumuachia huru winga kutoka nchini
Uholanzi Arjen Robben kutokana na kitendo cha kuukokota mpira kwa kipindi cha
sekunde kadhaa kabla ya kufanya maamuzi ya kupiga langoni na kusababisha bao lililowamaliza
kabisa.
Kwa matokeo hayo Man united wametupwa nje ya michuano ya
ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa jumla ya mabao manne kwa mawili.
0 comments:
Post a Comment