Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati alipokuwa akitoa taarifa ya kupitiwa upya kwa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu. Pamoja nae ni Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde (Kushoto) na Afisa Habari wa Idara ya Habari, Bibi Georgina Misana (Kulia).
Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde (Kushoto) akitoa ufafanuzi juu ya umuhimu wa kufanyiwa mapitio kwa Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu. Katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoks Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bi Joyce Mkinga na Afisa Habari wa Idara ya Habari, Bibi Georgina Misana (Kulia).
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bi Joyce Mkinga (katikati) na Mchambuzi Mkuu wa Sera (Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango), Bw. Edwin Ninde (Kushoto) wakiandika maswali yaliyokuwa yakiulizwa na wanahabari (hawapo pichani).
---
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS,TUME YA MIPANGO
1. Utangulizi:
Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu kwanza ya iliandaliwa mwaka 1992 ambapo ilifanyiwa na kuandaliwa upya mwaka 2006 kwa azma ya kuratibu na kushawishi sera za sekta nyingine, mikakati na program za maendeleo kuhakikisha zinajumuisha masuala ya maendeleo endelevu ya watu, kukuza usawa wa kijinsia, uwezeshaji wa wanawake, haki za watoto, na makundi mengine yenye uwezekano wa kuathiriwa kwa urahisi.
0 comments:
Post a Comment