Mlipuko
mkubwa wa bomu uliotokea katika soko moja mjini Islamabad Pakistan, umewaua
watu 23 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 50.
Tukio
hilo linaloonekana kama pigo kwa mazungumzo ya amani baina ya serikali na
wapiganaji wa kundi la Taliban, limetokea leo katika soko maarufu la matunda ya jumla wakati wachuuzi na
wanunuzi wakiwa wamekusanyika hapo kwa ajili ya biashara.
Mlipuko
huu ndio mlipuko mbaya zaidi kutokea katika mji huo tangu tukio la mlipuko wa
mwaka 2008 katika hoteli maarufu ya Marriott, na limetokea katika wakati ambao
serikali inajaribu kufanya juhudi za mazungumzo ya kukomesha uasi wa kundi la Tehreek-e-Taliban
Pakistan uliodumu kwa miaka saba sasa.
Kwa
mujibu wa Taasisi ya Sayansi ya Tiba nchini humo (PIMS) watu 50 wamejeruhiwa
katika mlipuko huo na wagonjwa wawili wana hali mbaya sana.
Tukio
hili linatokea mwezi mmoja baada ya shambulizi la bomu lililotokea kwenye jengo
la mahakama mjini Islamabad lililopoteza maisha ya watu 11 akiwemo jaji mmoja.
Pakistan
imekuwa ikitikiswa na mashambulizi yanayohusishwa na uasi wa kundi la Taliban
tangu mwaka 2007 lakini katika miaka ya hivi karibuni mashambulizi katika mji
mkuu yamepungua.
0 comments:
Post a Comment