WATU wanaotarajia kufunga harusi wametakiwa kujipanga kwa kufanya maandalizi mapema kwa kuwa siku hiyo ni muhimu katika maisha yao na haistahili kubezwa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Meneja Biashara na Maendeleo wa Kampuni ya 361, Hamis Omary inayojihusisha na maonesho ya harusi nchini.
Alisema watu hudhani harusi ni jambo la kawaida na wakati mwingine kupuuziwa lakini ni jambo kubwa kiimani na la kihistoria katika maisha linalopaswa kuungwa mkono na jamii.
Omary alisema maonesho ya harusi ambayo hufanywa na kampuni hiyo yametimiza mwaka wa tano ambapo mwaka huu yatafanyika kesho na kesho kutwa katika viwanja vya Parthenon.
Asema maonesho ya mwaka huu yameandaliwa na wabunifu mbalimbali na kwamba ni maonesho ya wazi hivyo kila mtu anakaribishwa kuhudhuria kujifunza mambo yanayohusu harusi na namna ya kuifanya siku ya harusi kuwa ya kuvutia.
0 comments:
Post a Comment