Polisi wa kutuliza ghasia mjini Cairo. |
Milipuko mitatu ya mabomu imetikisa katika Chuo Kikuu cha Cairo
nchini Misri na kuwaua watu 2 huku likiwajeruhi wengine kadhaa.
Maafisa wanasema kuwa raia mmoja na brigedia jenerali mmoja waliuawa
katika milipuko miwili ya awali.
Raia kadhaa na polisi watatu, akiwemo naibu mkuu wa polisi ni
miongoni mwa watu waliojeruhiwa.
Eneo la nje la chuo hicho limekuwa sehemu ya makabiliano
baina ya vikosi vya usalama na wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani,
Muhammed Mursi.
Serikali ya mpito nchini humo imewatupia lawama wafuasi hao,
lakini hakuna kundi lolote lililodai kuhusika na tukio hilo.
Mivutano nchini Misri imekuwa ikiongezeka tangu aliyekuwa
waziri wa ulinzi, Jenerali Abdul Fatah al-Sisi, kujiuzulu nafasi hiyo kwa lengo
la kutaka kugombea nafasi ya urais.
Mwaka 2012 al-Sisi aliteuliwa na Mursi kuwa mkuu wa jeshi na
waziri wa ulinzi. Lakini miezi kadhaa baadaye, alikuwa msitari wa mbele katika
harakati za kumuondoa Mursi madarakani.
Takwimu zinaonesha kuwa serikali ya sasa imewafunga watu
wapatao 16,000 ndani ya miezi kadhaa.
Mashirika ya kimataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu
yamekuwa yakielezea wasiwasi wake juu ya nguvu inayotumiwa na vikosi vya serikali
kuwadhibiti na kuwaua waandamanaji wanaipinga serikali.
Mashirika hayo yanasema kuwa kwa uchache watu 1,400 wameuawa
katika ghasia za kisiasa zilizoikumba nchi hiyo tangu kuondolewa kwa Mursi
madarakani, huku wengi wao wakiuawa kutokana na matumizi ya nguvu kupita kiasi
kutoka kwa vikosi vya usalama.
0 comments:
Post a Comment