Mzee Aboud Jumbe Mwinyi, Makamu wa Rais mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar ametangulia mbele ya Haki. Inna lillah waina ilaih raajiun.
Mzee Jumbe atakumbukwa katika historia ya Tanzania Kama
Kiongozi aliyeamini na kusimamia anachoamini bila kujali madhara yake.
Alipoteza nafasi zake za Uongozi Kwa sababu ya msimamo wake kuhusu muundo wa
Muungano kutoka Serikali 2 kwenda Serikali 3.
Mzee Jumbe ameacha maandiko kupitia kitabu chake cha The
Partnership ambacho ndugu yetu Ali Ally Saleh ' Alberto ' alipata heshima ya
kukifasiri.
Pia Mzee Jumbe ameacha ' memoir ' yake ambayo ninaamini
walioachiwa sasa wataweza kuitoa ili dunia ipate kujua mengi ambayo labda
hatujui kuhusu Nchi yetu.
Hivi hapa Tanzania kuna Hata barabara yenye jina la
Aboud Jumbe Mwinyi? Daraja? Nchi hii wakubwa wakigombana huwa hawasameheani?
Wazanzibari wanaweza kutumia msiba wa Mzee Jumbe kujenga
maridhiano na kuanza kujenga Zanzibar kwa pamoja?
0 comments:
Post a Comment