
Uturuki inajiandaa kufungua kambi yake ya kwanza ya
kijeshi barani Afrika ambapo maafisa wa kijeshi wa Uturuki watatoa mafunzo kwa
askari wa Somalia na vikosi mbalimbali kutoka mataifa mengine ya Afrika kwa
lengo la kupambana na kundi la Al-Shabaab, duru za kijeshi zimesema.
Kambi hiyo, ambayo imeidhinishwa na Umoja wa Mataifa,
itakuwa kambi ya pili ya jeshi la Uturuki nje ya mipaka ya taifa hili na
itawekwa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Kwa mujibu wa makubaliano baina ya serikali za Uturuki
na Somalia, zaidi ya vikosi 1,500 vya Kisomali vitapatiwa mafunzo na maafisa
200 wa jeshi la Uturuki.
"Kituo hiki cha mafunzo ya kijeshi kitakuwa kambi
muhimu katika kutoa mafunzo ya kejeshi kwa Afrika nzima,” afisa kutoka wizara
ya mambo ya nje ya Uturuki, Emil Tekin, alisema wiki iliyopita.
Afisa hiyo aliongeza kuwa Uturuki pia inapanga kujenga
shule ya kijeshi kwa lengo la kutoa mafunzo kwa maafisa wa ngazi za juu na wale
wa kawaida.
Uturuki imekuwa ikitoa msaada wa kijeshi wa Somalia
kupitia ushirikiano wa kijeshi na kiuchumi baina serikali mbili za mataifa hayo
kwa miaka mitano sasa.
Aidha, Uturuki iliipatia Somali zaidi ya dola milioni
400 katika kampeni kubwa ya huduma za misaada pindi ilipokuwa ikipambana
kulikabili baa la njaa.
Mwezi Desemba, Uturuki ilitangaza kuanzisha kambi yake
ya kwanza ya kijeshi nje ya mipaka yake. Kambi hiyo itakayowekwa nchini Qatar imepangwa
kuwa sehemu ya makubaliano ya kiulinzi yanayolenga kuzisaidia nchi hizo mbili
kukabilia na “adui wa pamoja”.
CHANZO: Daily Sabah
0 comments:
Post a Comment