Mawimbi mapya ya mapigano yameikumba Sudan Kusini tangu
Jumamosi baada ya vikosi vinavyomtii Rais Salva Kiir na vile vya upinzani
kupambana kusini magharibi mwa mji mkuu, Juba.
Matukio haya mapya yanafuatia mapigano mazito ya siku
tano yaliyoikumba Juba mwezi uliopita na kuua watu 300 huku maelfu wakiyakimbia
makazi yao.
Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa mapigano
mazito yalilipuka karibu na eneo la Yei, lililopo kwenye barabara
inayoiunganisha Juba na nchi jirani ya Uganda.
Mnamo Ijumaa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
liliidhinisha upelekaji wa kikosi maalum cha askari 4,000 nchini humo, ingawa serikali
ya Juba imendelea kushikilia msimamo wa kutohitaji askari wa kigeni.
Umoja wa Mataifa umetishia kuiwekea serikali ya Juba
vikwazo vya silaha iwapo itashindwa kutoa ushirikiano.
UNGANA NASI KATIKA WHATSAPP: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment