Donald Trump |
Mgombea wa Urais kupitia chama cha Republican nchini
Marekani, Donald Trump, amesema katika ujumbe wake mmoja wa Twitter kuwa ana
ushahidi unaoonesha kuwa maafisa katika Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA)
waliunga mkono na kusaidia mapinduzi ya kijeshi yaliyoshindwa nchini Uturuki.
Kauli yake hiyo inatarajiwa kuibua maneno makali katika
mpambano wa kampeni kati yake na mgombea wa chama cha Democratic, Hillary
Clinton.
Katika jumbe mbili mfululizo kwenye ukurasa wake rasmi
wa Twitter, Trump alisisitiza kuwa kuna ushahidi unaothibitisha kuwa maafisa 13
wa CIA waliwasaidia wale waliotaka kuipindua serikali ya Uturuki, na kwamba utawala
wa Obama uliruhusu kosa hili kubwa ambalo linagusa maslahi ya Marekani katika
eneo la Mashariki ya Kati.
Aidha, Trump aliongeza kuwa hivi karibuni atafichua
majina ya maafisa hao.
CHANZO: Mtandao wa politico.
0 comments:
Post a Comment