Wananchi wa Pakistan wakikurusha fataki kusherehekea
sikukuu ya uhuru wa nchi yao mjini Islamabad, Pakistan, Jumapili, Agosti 14,
2106.
|
Mamilioni ya wananchi wa Pakistan wanasherehekea
kumbukumbu ya miaka 70 ya uhuru kwa maandamano, fataki na kupandisha bendera nchini
kote.
Waziri Mkuu Nawaz Sharif amezielekeza sherehe hizo kama
zawadi kwa eneo la Kashmir lililogawanyika, huku Pakistan na India kila moja ikidai
kuwa lote ni milki yake. Kwa uchache watu 58 wamepoteza maisha kwa kupigwa
risasi na vikosi vya India ndani ya mwezi mmoja.
"Ninaitoa sikukuu ya leo kama zawadi kwa uhuru wa
Kashmir [inayokaliwa na India]. Ninaitoa zawadi kwa watu wale wanaokabiliana na
ukandamizaji wa dola kwa ushujaa mkubwa lakini wakaendelea kuhuisha moyo wa
kutaka uhuru,” Sharif alisema katika ujumbe wake wa siku ya uhuru.
Pia aliwakumbuka watu 70 waliouawa katika mlipuko wa
hivi karibuni kwenye hospitai moja katika mji wa Quetta kusini magharibi mwa
nchi hiyo, huku akiwakumbuka askari “waliotoa mhanga maisha yao kwa ajili ya
kuulinda uhuru huu.”
Zaidi ya Wapakistani 50,000, wakiwemo askari 5,000,
wameshapoteza maisha tangu nchi hiyo ilipojiunga katika kile kinachoitwa kama
Vita dhidi ya Ugaidi mwaka 2002.
Ungana nasi katika WhatsApp: +255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment