Mahakama nchini Misri imetoa hukumu ya kifungo cha miaka
mitatu jela kwa rais wa zamani wa nchi hiyo, Husni Mubarak, na wanaye wawili
kwa makosa ya ufisadi.
Kwa mujibu wa ripoti kutoka nchini humo, mahakama hiyo
imemtia hatiani Mubarak na wanaye wawili, Alaa na Gamal, kwa makosa ya
ubadhirifu wa fedha ya umma zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa
ikulu ya Rais.
Mahakama imetoa adhabu ya kifungo cha miaka mitatu kwa
kila mmoja, na kuwaamuru kulipa faini ya kiasi cha dola milioni 16.4, ambazo ndio
kiasi cha pesa zilizoibiwa.
Haijawa wazi iwapo uamuzi huo wa mahakama utaangalia
muda ambao watatu hao wameshautumia gerezani.
0 comments:
Post a Comment