Wananchi wa Croatia
wamepiga kura kwa wingi katika kura ya maoni ya kupiga marufuku ndoa za jinsia
moja, hatua inayonekana kuwa ni pigo kwa serikali iliyokuwa ipiga kampeni dhidi
ya mabadiliko hayo.
Matokeo rasmi ya awali
yanaonesha kuwa asilimia 65.76 wanataka katiba itamke wazi kuwa ndoa ni
“muungano baina ya mwanaume na mwanamke.”
Matokeo hayo
yatakapothibitishwa yatawekwa katika katiba na hivyo kuzipiga marufuku ndoa za
jinsia moja.
Aidha, matokeo hayo ni
pigo kwa Waziri Mkuu Zoran Milanovic na Rais Ivo Josipovic, ambao waliwataka
wananchi kupiga kura ya “hapana” kukataa mabadiliko hayo.
Baada ya Waziri Mkuu
kupiga kura yake, alisema kuwa kura hiyo ya ya maoni ni yenye kuhuzunisha na
isiyokuwa na maana.
Bunge la nchi hiyo
lililazimika kuitisha kura ya maoni baada ya zaidi ya wananchi 740,000 kusaini waraka unaotaka kuitishwa kwa
kura hiyo ya maoni.
Kampeni hiyo
ilianzishwa na kundi moja la wananchi na kuungwa mkono na chama cha upinzani
cha Croatian Democratic Union.
Kundi hilo lilitaka
tafsiri ya ndoa iwekwe katika katiba ili kwamba watu watakapotaka kufanya
mabadiliko watahitaji zaidi ya theluthi mbili ya kura za wabunge.
Hata hivyo, serikali ya
nchi hiyo imesema kuwa wiki chache zijazo itapeleka bungeni muswada wa sheria
utakaowapa haki zaidi wanandoa wa jinsia moja.
Baada ya ukamilishaji
wa mchakato huo, Croatia itaungana na kundi la nchi za Ulaya kama vile, Poland,
Belarus, Moldova, Bulgaria, Montenegro na Serbia, ambazo zimepiga marufuku ndoa
za jinsia moja katika katiba zao.
0 comments:
Post a Comment