Hatimaye mabaki ya miili ya wahanga 71 wa mauaji ya Srebrenica yamezikwa leo ikiwa ni kumbukumbu ya 22 ya mauaji makubwa kabisa ya kimbari
yaliyotokea barani Ulaya tangu mauaji ya Holocaust.
Mnamo Julai 11 mwaka 1995 zaidi ya Wabosnia 8,000, wengi
wao wanaume na vijana, waliuawa kinyama na wanajeshi wa Serbia kwa amri ya Jenerali
Ratko Mladić.
Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika kuomboleza mauaji
hayo huku ndugu na wanafamilia waliokuwa kwenye eneo la kumbukumbu la mauji
hayo nchini Bosnia wakibubujikwa na machozi kwa kuwapoteza ndugu na jamaa.
Baada ya swala ya adhuhuri, miili ya wahanga hao ambayo
ilitambuliwa mwaka jana baada ya kupatikana kwa makaburi ya pamoja katika
misitu na viwanda, ilizikwa katika eneo la makaburi la Potoçari.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres,
alitoa salamu zake za rambirambi kwa wanafamilia wa wahanga hao, na kuelezea
namna walinda amani wa Umoja huo walivyoshindwa katika jukumu lao walipopelekwa
huko.
Alisisitiza kuwa jumuiya ya kimataifa, na hasa Umoja wa
Mataifa, inabeba jukumu kwa masaibu hayo ya Srebrenista. Pia aliashiria kuwa
Umoja huo umekuwa ukiyafanya kazi mapungufu hayo na kujifunza kutokana na
makosa yaliyopita.
"Tunatakiwa kuyatazama kwa dhati yaliyopita,
kutambua uhalifu uliotokea na ubaridi uliosababisha yakatokea na kuhakikisha
kwamba mauaji kama hayo hayajirudii tena," alisema Guterres.
Mwaka 2007 mahakama ya Kimataifa ya Haki iliyatambua
mauaji hayo ya Srebrenica kuwa ni mauaji ya kimbari.
0 comments:
Post a Comment