WATU 56 WAUAWA NA 177 KUJERUHIWA NCHINI NIGERIA

This file photo taken on October 29, 2016 shows emergency personnel standing near the wreacked remains of a vehicle ripped apart following two suicide bombings in Nigeria. (AFP Photo)
Picha hii ya maktaba iliyopigwa Oktoba 29, 2016 inawaonesha wahudumu wa msaada wa dharura wakiwa wamesimama karibu na mabaki ya gari lililolipuliwa na milipuko ya bomu nchini Nigeria.  


Raia hamsini na sita wameuawa na wengine 177 kujeruhiwa katika milipuko miwili inayodhadhaniwa kuwa ni ya kujitoa mhanga katika mji wa Madagali kaskazini mashariki mwa Nigeria siku ya Ijumaa,kwa mujibu wa ripoti ya vyombo vya habari vya nchi hiyo.

Mwenyekiti wa Baraza la mji wa Madagali, Yusuf Muhammed, ameliambia Shirika la Habari la Nigeria kuwa watu 57 kati ya waliojeruhiwa wako katika hali mbaya, huku wengine 120 wakiwa na majeraha ya kawaida.

Msemaji wa jeshi mwanzo alikuwa amesema kuwa raia 30 walikuwa wameuawa na wengine 67 kujeruhiwa katika mlipuko huo.

Majeruhi walipelekwa hospitali katika miji ya Mubi na Gulak, Meja Badare Akintoye aliwaambia waandishi wa habari.

Akintoye alisema kuwa milipuko hiyo ilitokea katika soko moja la nafaka wakati wa asubuhi, na kwamba shambulizi hilo linadaiwa kutekelezwa na wanawake wawili waliojitoa mhanga.

Mji wa Madagali upo kilometa chache kutoka msitu wa Sambisa, unaoelezwa kuwa mmoja wa ngome kubwa kabisa za wanamgambo wa Boko Haram.

Mwaka 2014 mji huo ulitekwa na wanamgambo lakini baadaye mwezi Machi mwaka 2015 ulikombolewa wakati wa operesheni ya jeshi dhidi ya kundi hilo.



Wanamgambo hao wameongeza mashambulizi ya kujitoa mhanga na mashambulizi ya kushtukiza, hasa katika Jimbo la Borno ambako ndiko kundi hilo lilikozaliwa ambapo mapema wiki hii ripoti imetolewa ripoti kuwa kiasi cha raia 240 wameshauawa ndani ya mwaka huu. Aidha, jeshi nalo limewapoteza maafisa na askari muhimu katika mashambulizi yaliyotekelezwa na kundi hilo la wanamgambo.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment