Bwana harusi akitoka chooni huku mabibi harusi wakisubiri wakati wa shughuli ya ndoa za pamoja iliyowashirikisha maharusi 92 katika viwanja vya Ramlila mjini New Delhi Juni 15, 2014. |
Mahakama moja nchini India imempa mwanamke mmoja ruhusa ya
kuachana na mumewe kwa sababu nyumba yao haina choo, hali inayowalazimu
kujisaidia nje.
Mahaka hiyo ya masuala ya kifamilia katika jimbo la kaskazini
magharibi la Rajasthan ilitoa hukumu hiyo siku ya Ijumaa kwa kumtetea mwanamke
huyo ambaye alitoa hoja kuwa kitendo cha mumewe kushindwa kujenga choo kwa
kipindi cha miaka mitano ya ndoa yao ni sawa na ukatili.
Jaji Rajendra Kumar Sharma alisema kuwa wanawake katika vijiji
mbalimbali mara nyingi hukumbwa na maumivu ya mwili wakisubiri giza litande ili
wapate kujisaidia sehemu za wazi.
Jaji huyo alikiita kitendo cha kujisaidia nje kuwa cha fedheha
na mateso kwa kuwa kinawanyima wanawake mazingira salama ya kujisaidia.
Nchini India talaka hutolewa iwapo mahakama itapokea uthabitisho
wa ukatili, dhulma au kushindwa kutimiza mahitaji ya mke.
Ni mara ya kwanza ndoa inavunjwa kwa sababu za ukosefu wa choo.
Mnamo mwezi Juni, mwanamke mmoja alikataa kurudi kwa wakwe zake
mpaka wajenge choo.
Mnamo mwaka 2016, mwanamke mwingine alikataa kufunga ndoa katika
jimbo la Uttar Pradesh baada ya mchumba wake kukataa kujenga choo
watakachotumia.
NI TATIZO MTAMBUKA
Takribani nusu ya wakazi wa India – karibu milioni 600 — hujisaidia
maeneo ya wazi, kwa mujibu wa shirika la UNICEF.
Kiasi cha asilimia 70 ya kaya
za India hazina vyoo, ingawa asilimia 90 zina huduma ya simu za mkononi.
Waziri Mkuu wan chi hiyo, Narendra
Modi ameahidi kujenga choo kwa kila nyumba mpaka kufikia mwaka 2019 katika
hatua za kukomesha mazoea ya kujisaidia nje.
Serikali inasema kuwa vyoo milioni 20 vimejengwa tangu kuanza
kwa mpango huo mwaka 2014.
Lakini wataalamu wanasema kuwa mazoea ya kujisaidia nje sio tu
kwamba yanatokana na umasikini bali ni imani kwamba vyoo vya ndani ya nyumba
husababisha uchafu.
Wanaharakati wanakadiria kuwa takriban watoto wachanga 200,000 hufariki
dunia kia mwaka kutokana na maambukizi yatokanayo na kujisaidia nje, hali
ambayo inasemekana pia kwamba huwafanya wanawake kuwa katika hatari ya kubakwa.
Mwanaume akikojoa kwenye ukuta pembezoni mwa barabara mbele ya bango la filamu ya kihindi ya "Choo- Hadhithi ya Mapenzi" katika mji wa kusini wa Hyderabad mnamo Agosti 12, 2017. |
"CHOO: HADITHI YA MAPENZI"
Suala hilo limekuwa kubwa pia katika medani ya filamu za India, maarufu kama Bollywood.
Mapema mwezi huu, Bollywood ilitoa filamu iliyoitwa Toilet: Ek Prem Katha (Choo: Hadithi ya Mapenzi) ambayo inatokana na kisa cha kweli cha mwanaume mmoja anayepambana kujenga vyoo katika kijiji chake nchini India.
Alitaka kumrejesha mkewe nyumbani kwake, ambapo kitendo chake
cha kukataa kuishi katika nyumba isiyokuwa na choo ilisifiwa na kupongezwa
nchini humo.
Waandishi
wa muswada wa filamu hiyo, Siddharth Singh na Garima Wahal, wanasema kuwa wana
matarajio kwamba filamu hiyo
iliyomshirikisha mmoja wa nyota wakubwa wa tasnia ya filamu nchini humo,
Akshay Kumar, itakuwa na “taathira halisi” katika jamii ya India.
"Hii ilitokea katika kijiji kimoja huko Madhya Pradesh, na tulidhani kuwa lilikuwa ni jambo kubwa sana," anasema Singh, akikusudia moja ya majimbo yenye hali duni nchini humo.
Waandishi hao wanasema kuwa walikutana na visa kadhaa vya
wanawake wanaoshambuliwa pindi walipokwenda mashambani wakati wa usiku mwingi
katika mchakato wa utafiti wa filamu hiyo.
Kumar,
ambaye ni mmoja wa waigizaji wanaolipwa pesa nyingi sana duniani akiwa na
kipato cha dola milioni 31.5 kwa mujibu wa orodha ya jarida la Forbes
iliyochapishwa mwaka 2016, hivi karibuni alitoa “Wimbo wa Choo” ili kufanya
kampeni ya jambo hilo.
"Wakati binadamu ameendelea kiasi cha kusafiri kwenda
kwenye sayari ya Mars na kupanda mlima Everest, asilimia 54 ya watu wa India
wanajisaidia sehemu za wazi,” unasema wimbo huo.
0 comments:
Post a Comment