Waziri Mkuu wa Kazakhstan aliyejiuzulu, Serik Akhmetov. |
Waziri Mkuu wa Kazakhstan, Serik Akhmetov amejiuzulu
yeye pamoja na serikali yake yote.
Akhmetov aliliambia baraza la mawaziri kuwa Rais wa nchi
hiyo Nursultan Nazarbayev amempa Baraka zote katika uamuzi wake huo.
Hakuna sababu maalumu iliyotolewa juu ya hatua hiyo,
lakini Rais Nazarbayev ana nguvu kubwa ya kubadilisha mawaziri wakuu kwa kadiri
apendavyo.
Idara ya habari katika ofisi ya ikulu imetoa taarifa
katika mtandao wa Twitter kuwa kiongozi wa nchi huyo ameshampendekeza aliyewahi
kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Karim Masimov kuchukua tena wadhifa huo.
Kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo, Waziri Mkuu
anapojiuzulu hulifanya baraza lote la mawaziri kuvunjika.
Akhmetov mwenye umri wa miaka 55, aliwahi kufanya kazi
katika sekta ya chuma ya nchi hiyo kabla ya kuteuliwa kuwa naibu meya wa mji
mkuu wa nchi hiyo, Astana.
Alishika nyadhifa mbalimbali serikalini na hatimaye
mwaka 2012 aliteuliwa kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo akimrithi Masimov, ambaye
aliutumikia wadhifa huo kwa muda wa miaka 5.
Kazakhstan inapatikana katika eneo la katikati mwa bara
la Asia na ni mzalishaji mkubwa wa mafuta duniani.
0 comments:
Post a Comment