Pervez Musharraf, Rais wa zamani wa Pakistan. |
Rais wa zamani wa Pakistan Pervez Musharraf amenusurika
jaribio la kuuawa. Kwa mujibu wa taarifa kutoka nchini humo, msafara wake
ulinusurika shambulizi la mlipuko mjini Islamabad.
Tukio hilo limetkea siku chache baada ya mkuu wa jeshi
la nchi hiyo Jenerali Raheel Sharif kuishauri
serikali imruhusu Musharraf, aliyehukumiwa kwa uhaini, kusafiri nje ya nchi kwa
ajili ya matibabu na kumuangalia mama yake ambaye ni mgonjwa.
Suala hilo la Musharraf mwenye umri wa miaka 70
lilijadiliwa wakati wa kikao baina ya Jenerali Raheel na Waziri Mkuu Nawaz
Sharif. Mkuu wa shirika la upelelezi la nchi hiyo, Luteni Jenerali Zaheerul
Islam naye alihudhuria kikao hicho cha kuamua mustakbali wa Rais huyo wa
zamani.
0 comments:
Post a Comment