Suns 94,
Pelicans 88
Kazi kubwa iliyofanywa na walinzi wa timu ya Phoenix
Suns katika mchezo wa ligi ya mpira wa kikapu ya nchini Marekani (NBA) Gerald
Green pamoja na Goran Dragic iliisaisdia timu hiyo kujiongezea point 41 miongoni
mwa point 94 ambazo ziliwatoa nishai New Orleans Pelicans.
Mchezo huo ambao umechezwa mishale ya alfajiri kwa
saa Afrika mashariki ulishuhudia Eric Bledsoe akifunga point 16 pekee yake
katika kipindi cha pili cha mchezo huo, na kuibua matumaini ya ushindi ambao
wameupata.
Ushindi huo umewaweka Phoenix Suns katika mazingira mazuri ya
kucheza hatua ya mtoano kwenye ligi hiyo, huku wakiwa mbele kwa mchezo mmoja
dhidi ya Memphis
- - -
Grizzlies
107, Heat 102
Grizzlies walipata nguvu ya kutosha
kutokana na uwezo binafsi ulionyesha na baadhi ya wachezaji wao Zach Randolph,
Mike Conley pamoja na Marc Gasol ambao kwa pamoja waliifungua timu hiyo point 71
katika mchezo dhidi ya Miami Heat.
Katika mchezo huo wachezaji hao
watatu walifanikiwa kucheza mipira iliyokua inarudi (rebounds) 28 na hivyo
kuifanya Memphis kuendeleza matumaini ya kucheza hatua ya mtoano.
Mshambulaiji wa Miami LeBron James alifanikiwa
kufunga point 37 ambazo hata hivyo hazikuweza kuisaidia timu yake kupata
ushindi, japo kuna wakati aliiweka mbele kwa kuongoza point 53-25.
- - -
Pacers
104, Bucks 102
Chris Copeland alifanikiwa kufunga
point 18 ambazo ziliisaidia timu yake ya Indiana Pacers kuibuka na ushindi wa
point 104-102 dhidi ya Milwaukee Bucks.
Indiana walipata ushindi katika
mchezo huo, ikiwa kama faraja kwao, baada ya kupoteza michezo miwili mfululizo,
ambayo ilishuhudiwa wakicheza bila wachezaji wao watano muhimu.
Ushindi huo ulipatikana baada ya Indiana
Pacers kuongoza kwa point 54-25 hali ambayo iliongeza morari kwa wachezaji wa
timu hiyo kuwa mbele mpaka mwishoni mwa mchezo huo.
- - -
Hawks 105,
Celtics 97
The Atlanta Hawks walifanikiwa kutoka
nyuma kwa point tisa na kushinda mchezo huu, dhidi ya wapinzani wao Boston
Celtics ambao walionekana kucheza vyema zaidi katika kipindi cha kwanza.
Jeff Teague aliweka rekodi ya
kufunga point 19 huku akisaidia kutoa pasi mara nane ambazo zilimpa nafasi,
Kyle Korver kufunga point 17 hali ambayo
imeipa ahuweni timu ya Atlanta Hawks
kusogea katika nafasi ya nane katika msiamo wa ligi ya NBA ukanda wa mashariki.
Kufuatia hali hiyo Atlanta Hawks
itawalazimu kuendeleza wembe wa ushindi katika michezo yao miwiwli inayofuata
dhidi ya Nets Brooklyn pamoja na Miami Heat ili wakamilishe azma yao ya kutinga
katika michezo ya hatua ya mtoano.
- - -
Nuggets
123, Rockets 116
Randy Foye amefanikiwa kufunga point
30 huku akisaidia kutoa pasi zilizo zalisha point nyingine 22 zilizofungwa na Kenneth
Faried na kuifanya Denver Nuggets kuizamisha Houston Rockets.
Kwa upande wa Houston Rockets,
Jeremy Lin alifanikiwa kufunga point 18 akifuatiwa na Chandler Parsons aliyefunga
point 16 ambapo hata hivyo haikuisadia timu hiyo kuendeleza wimbi la ushindi
kama ilivyokuwa katika michezo mitatu iliyopita.
- - -
Bobcats
94, Wizards 88
Al Jefferson alifunga point 20 ambapo
kati ya point hizo 18 ziliotokana na mipira iliyokua inarudi huku Kemba Walker akifunga
point 17 ambazo ziliwaongezea morari Charlotte Bobcats kuwaangusha Washington
Wizards katika mchezo wao watano kushinda mfululilizo.
Gary Neal alifanikiwa kuifungia
Wizards point 16 wakati Bobcats wakiongoza kwa point 40-38.
Matokeo ya
michezo mingine iliyochezwa alfajiri ya hii leo kwa saa za Afrika mashariki ni
kwamba:
Bulls 102,
Timberwolves 87
Magic 115,
Nets 111
Cavaliers
122, Pistons 100
Raptors
125, 76ers 114
0 comments:
Post a Comment