MUGABE: WANAOSUBIRI NIFE IMEKULA KWAO

Photo by: Reuters
Rais Robert Mugabe ahutubia wafuasi wa chama chake cha ZANU (PF) waliokusanyika mjini  Chinhoyi, Zimbabwe, Julai 29, 2017. 

Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe mapema Jumamosi alisema kuwa hataondoka madarakani wala kufa na kwamba hakuna yeyote katika chama chake ambaye anaweza kushika madaraka mapema kutoka kwake.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 amekuwa madarakani tangu nchi hiyo ilipojipatika uhuri wake kutoka kwa Waingereza mwaka 1980. Afya yake inafuatiliwa kwa karibu na raia ambao wanahofu kwamba nchi hiyo inaweza kutumbukia katika ghasia iwapo atafariki bila kumteua atakayemrithi.

Mugabe aliwaambia makumi kwa maelfu ya wafuasi wake kwenye mkutano wa hadhara katika mji aliozaliwa wa Chinhoyi, kwamba hivi karibuni madaktari walistaajabishwa na “uimara wa mifumo wa mifupa” yake.

Mwaka huu amesafiri kwenda Singapore kwa kile ambacho maafisa wanasema ni safari za kawaida za kimatibabu.

"Kuna minong’ono kwamba rais anaachia ngazi. Siondoki," Mugabe aliwaambia wafuasi wake kwenye viwanja vya chuo kikuu katika eneo hilo, kilometa 100 (maili 60) magharibi mwa mji mkuu Harare.

"Wanasema rais anakufa. Sifi. Nitakuwa na maradhi ya hapa na pale lakini mwili na viungo vyangu vyote vya ndani ni imara sana, tena sana," Mugabe alisema.

MGAWANYIKO NDANI YA CHAMA

Suala la mrithi wa Mugabe limesababisha mgawanyiko mkubwa ndani ya chama tawala, ambapo kundi moja linamuunga mkono Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa na la pili linamuunga mkono mke wa Mugabe, Grace Mugabe.

Mnamo Alhamisi, Grace alimtaka Mugabe kumteua mrithi wake anayemuamini ili kukomesha mgawanyiko kuhusu mustakbali wa uongozi ndani ya chama tawala cha ZANU-PF.

Alirudia wito wake siku ya Jumamosi na kuongeza kuwa Mugabe mwenyewe ndiye atakayeongoza mchakato wa kumchagua mrithi wake.


Hata hivyo, Mugabe alisema kuwa ingawa baadhi ya vigogo wa chama wanataka kumrithi, lakini hajaona yeyote atakayekifanya chama hicho kubaki katika hali ya umoja na kukabiliana na upinzani wa chama kikuu cha upinzani cha Movement for Democratic Change (MDC).
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment