Picha hii iliyopigwa Julai 2, 2017 ikionesha mtaa
uliokumbwa na mafuriko katika eneo la Loudi, katika jimbo la Hunan.
|
Mafuriko na maporomoko ya ardhi vimeua watu kadhaa
katika jimbo la Hunan katikati mwa China kufuatia mvua zilizowafanya watu
milioni 1.6 kukosa makazi, mamlaka nchini humo zimesema.
Kiasi cha nyumba 53,000 zimeanguka huku kiasi cha
nyingine 350,000 zikiharibiwa vibaya baada ya mvua iliyonyesha kwa muda wa siku
11 mfululizo, kwa mujibu wa Tang Biyu, naibu mkurugenzi wa kitengo cha huduma
za kijamii katika jimbo hilo.
Kwa uchache watu 63 waliuawa na maporomoko ya ardhi,
maporomoko ya vifusi au nyumba zilizoanguka, huku kiasi cha 20 wakiwa
hawajulikani waliko, almesema Tang katika taarifa yake ambayo ilieleza kuwa
hasara iliyotokana na mvua hiyo ni kiasi cha dola bilioni 5.6.
Maeneo ya katikati na kusini mwa China yamekumbwa na
gharika tangu mwezi jana.
Wiki iliyopita, mamlaka katika mkoa wa kusini wa Guangxi
ziliripoti kuwa watu zaidi ya ishirini walipoteza maisha au kupotea katika
mafuriko ambayo pia yaliharibu maelfu ya makazi.
Mwishoni mwa mwezi Juni, maporomoko makubwa ya ardhi
yalikizika kijiji katika jimbo la kusini magharibi la Sichuan, yakaua watu
wasiopungua 10 na kuwaacha wengine 73 wakiwa hawajulikani waliko.
0 comments:
Post a Comment