Rais John Magufuli ameukumbuka mchango wa marais
wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete na kuwashukuru huku akieleza kuwa
wao ndiyo waliotengeneza maisha yake ya kisiasa hadi kuwa kiongozi.
Magufuli ameyasema hayo leo Jumatatu, Julai 10 wilayani
Chato wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa
Foundation.
“Nakumbuka siku hiyo tulikuja hapa Chato na wewe (Mkapa)
Msafara ulisimamishwa na ukawaambia wananchi wa Chato nichagulieni huyu,
nakumbuka ulikuwa umevaa viatu vyekundu,” amesema na kuongeza:
“Kwa bahati nzuri, wananchi wa Chato wakanichagua,
baadaye ukanichagua kuwa naibu waziri. Wewe ulinitangaza, sikustahili chochote,
maneno yako yalikuwa na nguvu kwa Watanzania.”
Amesema anamkushukuru pia Rais Mstaafu Jakaya Kkwete na
kusema: “Baada ya kipindi cha Mkapa, Kikwete alipokuja, lakini kwanza wewe
ukanipitisha kugombea ubunge tena kwa mara nyingine, nikachaguliwa bila
kupingwa katika jimbo hili.” Amesema
Amesema hata katika kipindi cha awamu ya nne, Rais
Kikwete alimteua katika wizara mbalimbali.
“Kwangu mimi nyinyi mlitengeneza maisha yangu katika
uongozi. Pia nawashukuru sana viongozi wa awamu ya kwanza, Nyerere na Mwinyi
ambao walitengeneza mazingira mazuri ndani ya Chama cha Mapinduzi,” amesema na
kuongeza:
“Kwangu mimi sina cha kuwalipa jukumu langu ni kuwatetea
na ninawaahidi Watanzania kuwa nitafanya kazi kwa nguvu zangu zote, namuomba
Mungu asinifanye nikawa na kiburi namuomba asinifanye nikasahau nilipotoka.”
0 comments:
Post a Comment