Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Saimon Sirro, amefanya mabadiliko ya Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani pamoja na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya.
Katika mabadiliko hayo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi
Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi Mohamed Mpinga anaenda kuwa Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Mbeya, na nafasi yake inachukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa
Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.
Aidha, Aliyekuwa
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao
Makuu ya Upelelezi.
Uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa
kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.
Imetolewa na:
Barnabas D. Mwakalukwa – ACP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
Makao Makuu ya Jeshi la Polisi.
0 comments:
Post a Comment