Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia huru
aliyekuwa Kamishna wa TRA, Tiagi Masamaki na Wenzake watano waliokuwa
wakishtakiwa na makosa ya uhujumu uchumi na kuisababishia serikali hasara ya
sh. Bilioni 12.7.
Washtakiwa hao wameachiwa na Hakimu Mkazi Huruma Shahidi
baada ya upande wa mashtaka uliokuwa ukiongozwa na wakili wa Serikali
Mwandamizi, Timon Vitalis kuiomba mahakama kufanya hivyo chini ya kifungu cha
91(1) ya makosa ya jinai (CPA) kuwa DPP
hana nia ya kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa hao.
"Mheshimiwa Hakimu kesi hii leo imekuja kwa ajili
ya kutajwa, hata hivyo tuna maombi, DPP amewasilisha Nolle Prosque, hana nia ya
kuendelea na mashtaka dhidi ya washtakiwa", amesema Wakili wa Serikali
Timon Vitalis.
Hakimu Shahidi alikubaliana na ombi hilo na kuwaachia
huru washtakiwa.
Mbali na Masamaki, washtakiwa wengine waliokuwa katika
kesi hiyo iliyotokana na sakata la
makontena 329 ni Meneja Kitengo cha Huduma za Ushuru TRA, Habib Mponezya (45) na Meneja Msimamizi na Ufuatiliaji wa
Forodha, Burton Mponezya (51).
Msimamizi Mkuu Kitengo cha Ushuru wa Forodha ICD Azam, Eliachi Mrema (31),
Mchambuzi Mwandamizi wa Masuala ya Biashara TRA,
Hamis Omary (48), Meneja wa Oparesheni
za Usalama na Ulinzi ICD, Raymond
Adolf Louis (39) na Meneja wa Azam ICD, Ashrafu Khan (59) na Haroun Mpande (28)
wa kitengo cha Mawasiliano ya Kompyuta ICT TRA.
Hata hivyo, DPP amewafutia mashtaka watuhumiwa watano tu
ambao ni,Tiagi Masamaki, Eliachi Mrema, Habibu Mponezya, Burton Mponezya na
Ashraf Khan.
Hata hivyo, Raymond Louis, Haruni Mpande na Khakis Ally
Omari wameendelea kushikiliwa na kusomewa mashtaka mapya pamoja na watuhumiwa
wapya, Khalid Yusuph Hassan na Benson Vitalis Malembo.
0 comments:
Post a Comment