Ghana imetuma angani satelaiti yake ya kwanza tangu
ilipojipatia uhuru. Satelaiti hiyo ya GhanaSat 1, ilitengenezwa na wanafunzi wa
Chuo Kikuu cha All Nation cha nchini humo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, GhanaSat-1,
iliyorushwa kutoka kituo cha anga cha kimataifa, pamoja na mambo mengine itatumika
kwa tafiti za sayansi na mafunzo ya masuala ya anga nchini humo na Afrika kwa
ujumla.
Kwa mujibu wa mratibu wa mradi huo, Dk Richard Damoah,
satelaiti hiyo pia itasaidia kutoa mafunzo kwa kizazi kichanga juu ya namna ya
kutumia satelaiti kwenye shughuli mbalimbali katika bara zima.
Uzinduzi huo wenye mafanikio umeiweka Ghana kwenye
ramani ya kimataifa kama nchi ya kwanza katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara
kutuma satelaiti ya kimafunzo angani.
Rais wan chi hiyo Akufo-Addo amekipongeza Chuo Kikuu cha
All Nations University kwa kufanikisha mradi huo.
0 comments:
Post a Comment