WAGOMBEA sita wamepitishwa kugombea urais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12,
mwaka huu katika hatua za awali.
Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Kamati ya
Uchaguzi, msomi Wakili Revocatus Kuuli alitaja wagombea hao kuwa ni Shija
Richard, Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay na
Emmanuel Kimbe.
“Kikao kimekaa leo na kimepitisha majina ya wagombea kwa
hatua ya awali na majina yote yatabandikwa kwenye mbao za matangazo kuanzia
kesho ,” alisema Wakili Kuuli.
Awali wagombea kumi walichukua fomu kuwania nafasi ya
urais lakini mapema Athuman Nyamlani alijitoa hivyo majina ambayo
hayakupitishwa ni Fredrick Masolwa, Jamal Malinzi na John Kijumbe kwa sababu
mbalimbali.
Katika nafasi ya Makamu wa rais waliopitishwa ni Mulamu
Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Stephen Mwakibolwa na Robert
Selasela huku Geofrey Nyange akielezwa kujitoa.
Katika nafasi ya wagombea wa nafasi ya kamati ya
Utendaji Kocha mwenye maneno mengi Jamhuri Kihwelo, Bakari Malima, Abdallah
Mussa, kwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kuthibitisha elimu ya sekondari kwa
mujibu wa kanuni ya 9(2) za uchaguzi.
Wagombea ambao hawakupitishwa kwa kukosa uzoefu kwa
mujibu wa kanuni ya 9(3) ni Musa Sima, Salehe Alawi, Thabith Kandoro na Hassan
Othuman hajapitishwa kwa kukosa uadilifu kwa mujibu wa kanuni ya 9(7) za
uchaguzi wa TFF.
Zoezi la kuchukua fomu lilianza Juni 16, 2017 hadi Juni
20, mwaka huu na jumla ya wagombea 74
walichukua na kurudisha fomu kuomba kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi
huo.
Awali mchujo ulianza Juni 23, kwa mujibu wa kanuni ya
11.1 ya Uchaguzi wa TFF lakini kulitokea kutokuelewana kati ya mwenyekiti wa
kamati hiyo Wakili Kuuli na wajumbe wa kamati hiyo hali iliyofanya Kuuli
kujiuzulu kabla ya Kamati ya Utendaji ya TFF kukaa na kuivunja kamati hiyo na
yeye kurejeshwa tena peke yake.
(Habari kwa hisani ya mtandao wa Lenzi ya Michezo)
UNGANA NASI:
WhatsApp: +255 626 603 852
0 comments:
Post a Comment