Jeshi la Uganda limesema kuwa
askari wake 12 waliuawa na wanamgambo wa al-Shabaab katika shambulizi ya
kuvizia siku ya Jumapili kusini mwa Somalia.
Wizara ya Ulinzi ya Uganda
imesema katika taarifa yake leo kuwa askari wengine wanane walijeruhiwa katika
shambulizi hilo lililotokea katika mkoa wa Sabelle ya chini.
Vikosi vya Uganda viko nchini
Somalia kama walinda amani chini ya mwavuli wa Umoja wa Afrika. Mamlaka za
Uganda zinasema kuwa shambulizi hilo lilitokea wakati wakifanya doria ya pamoja
na vikosi vya Kisomali.
Mpaka sasa hakuna kauli yoyote kuhusu vifo kwa upande wa askari
wa Somalia.
Al-Shabaab wanadai kuwa waliua
askari 39.
Shambulizi hilo lilitokea saa
chache baada ya bomu lililolipuka mjini Mogadishu na kuua watu wasiopungua watu
watano, wengi wao wakiwa raia, na hivyo kuondosha hali ya utulivu iliyodumu kwa
muda wa mwezi mmoja katika mji huo.
0 comments:
Post a Comment