Bila shaka ni hakika kwamba duniani vituko havitakwisha.
Nchini Hispania watu hufanya tamasha la kila mwaka la mazishi.
Wale ambao siku za karibuni walinusurika kufa, hubebwa
katika majeneza ya wazi na kutembezwa katika mji mdogo wa Galicia nchini humo.
Tukio hilo la kila mwaka ni maalum kwa wale ambao
walikaribia kufa na wakataka kutoa heshima zao kwa mtakatifu wa mji huo, Santa
Marta. Wale wanaoshiriki katika ibada hiyo humuomba na kumshukuru mtakatifu
huyo.
Wakati wa matembezi, washiriki huimba nyimbo za kidini
na kubeba mishumaa huku wakitembea kwa magoti yao kuonesha utii wao.
Maelfu ya watu kutoka Hispania na Ureno hukusanyika kutazama
maadhimisho hayo kila mwaka, ambayo inaaminika yalianza tangu karne ya 17.
0 comments:
Post a Comment