Baada ya muongo mmoja akiwa madarakani, rais wa kwanza
mwanamke kuchaguliwa kuwa r’ais barani Afrika, Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf,
anatarajiwa kung’atuka madarakani baada ya uchaguzi wa urais utakaofanyika
mwezi Oktoba.
Kuna jumla ya wagombea 20 wanaowania kumrithi mwanamama
huyo, lakini hakuna mgombea anayeonekana kuwa kinara. Hata hivyo, mcheza soka
maarufu wa zamani George Weah, aliyeshindwa na Bibi Ellen Srleaf katika
uchaguzi wa mwaka 2005 anatarajiwa kutupa karata yake tena.
Mbali na Weah, mbabe wa vita wa zamani Prince Johnson naye
anatarajia kugombea.
Rais wa sasa wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf |
Vyombo vya habari vinasema kuwa katika orodha hiyo kuna
mwanamke mmoja tu, naye ni MacDella Cooper, aliyewahi kuwa manamitindo, lakini
kwa sasa anajishughulisha na utoaji wa huduma za kiutu.
Hii itakuwa mara ya pili kwa George Weah kuwania kiti
hicho.
0 comments:
Post a Comment