BARAZA LAMPA AMRI YA KUMUOA PUNDA NA KUMTUNZA MAISHA YAKE YOTE

حمار

Ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni. Kila siku maajabu
mapya yanaibuka katika dunia yetu hii na kushangaza ulimwengu.

Baraza moja la kimila nchini Afrika Kusini limetoa hukumu dhidi ya jamaa mmoja na kumuamuru kumuoa punda baada ya jamaa huyo kufumaniwa akimnajisi punda huyo katika shamba moja la jirani.

Mmiliki wa shamba hilo alimkamata jamaa huyo katika wilaya ya Limpopo akifanya mapenzi na punda huyo, akatoa taarifa kwa wazee wa kimila katika tukio hilo ambalo sio la kwanza.

Mmiliki huyo alisema: “Nilipomuona akimbaka punda alinitaka radhi lakini sikumkubalia kwa sababu sio mara ya kwanza kwake kufanya kitendo hicho”.

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kuwa baraza hilo la kimila lilimpa adhabu jamaa huyo ya kumuoa huyo punda na kumtunza kwa kipindi chote cha uhai wake.

Taarifa hiyo inasema kuwa licha ya hukumu hiyo, mtuhumiwa atatakiwa kufika mbele ya mahakama rasmi ya kimila ili kusikiliza mashitaka dhidi yake.


Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment