Shule ya kwanza ya uchawi na uganga imeanzishwa barani
Afrika. Jukumu la shule hiyo, pamoja na mambo mengine, ni kutengeneza wataalamu
wabobezi katika masuala ya uchawi na uganga huku wahitimu wakipewa vyeti rasmi.
Shule hiyo itakuwa chini ya usimamizi wa wizara ya elimu.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo, waziri wa
elimu wa nchi hiyo, Blade Nzimande, ametangaza kuwa shule hiyo maalumu kwa
mafunzo ya uchawi ilifungua milango yake tangu tarehe 20 Machi, na itaanza
kupokea wanafunzi wake wa mwanzo mwaka huu.
Ili kutilia nguvu hoja ya uanzishwaji wa shule hiyo ya
aina yake, waziri huyo alisema kuwa serikali imechoshwa na watu wanaofanya
uchawi bila ithibati na vibali, huku akiifananisha fani hiyo na fani za
uhandisi, udaktari na ukasisi ambazo wataalamu wake huenda vyuo vikuu ili
kuongeza ujuzi na utaalamu wao. Akasema kuwa waganga wanaotibu kwa uchawi
wanatakiwa kujiendeleza kimafunzo ili waweze kutumia vizuri vipaji na vipawa
vyao. Hivi karibuni fomu za kujiunga na masomo hayo zitapatikana kwenye tovuti
rasmi ya shule hiyo.
Ripoti ya mtandao huo imesema kuwa, pamoja na elimu ya
uganga na uchawi, shule hiyo ya aina yake barani Afrika itatoa kozi za hisabati
za fizikia.
CHANZO: Ram News
0 comments:
Post a Comment