Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, amekiri kuwa “uvamizi”
uliofanywa na majeshi ya kigeni dhidi ya utawala wa Kanali Muammar Gadhafi
mwaka 2011 lilikuwa kosa huku akisema kuwa Ufaransa ilifanya kosa kushiriki
vita hiyo.
Rais Macron amesema katika taarifa moja kuwa “uingiliaji
kati wa nchi za Magharibi lilikuwa kosa”.
Itakumbukwa kuwa mwaka 2011, Ufaransa chini ya rais Nicolas
Sarkozy, ilikuwa kinara wa kuchochea uvamizi dhidi ya Libya na kulifanya Baraza
la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kutoruhusu ndege za Libya
kuruka.
Ndege za Umoja wa Kujihami wa nchi za Mgharibi, NATO,
ikiwemo Ufaransa, ziliishambulia nchi hiyo ya Afrika Kaskazini na kuwatuma
askari kwa lengo la kuwasaidia waasi kumuondosha madarakati Kanali Muammar
Ghaddafi.
Ghaddafi aliuawa lakini mambo yakawa mabaya zaidi.
Nchi za Magharibi ziliondoka na kuliacha jeshi la nchi
hiyo likiwa taabani. Ombwe la usalama na kuzaa kwa silaha vilichochea kuibuka
kwa makundi ya wanamgambo yaliopambana kutaka madaraka na mali.
Hali hii ya ukosefu wa uthabiti ilitengeneza mazingira
salama kwa makundi ya kigaidi. Makundi hayo yalitumia fursa ya mapigano na
mzozo wa ndani kati ya mirengo ya kisiasa na wanamgambo.
Kutokana na kutawaliwa na jangwa kwa sehemu kubwa na
kuwa karibu na Ulaya kwa njia ya bahari, Libya imekuwa kivutio kwa walanguzi na
safari za wahamiaji. Mambo yote hayo yamekuwa tishio dhidi ya uhai wa dola ya
Libya.
Urejeshaji wa amani na uthabiti imekuwa ndoto.
Macron amekiita kitendo cha uvamizi wa mataifa ya
Magharibi nchini humo kuwa ni kosa. Lakini sio kosa la kwanza; kwani kosa kama
hilo lilifanyika Iraq baada ya kuanguka kwa Saddam Hussein.
0 comments:
Post a Comment