Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (kulia), akizungumza katika mkutano na
waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa taarifa ya kupungua kwa
bei za dawa, vifaa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara kutokana na uamuzi
wa serikali wa kununua moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu.
Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu akisisitiza jambo katika mkutano huo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye mkutano huo.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala wa MSD, Victoria
Elangwa, Mkurugenzi Mkuu MSD, Laurian Bwanakunu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu,
Kaimu Mfamasia Mkuu wa Serikali kutoka Wizara ya Afya, Siana
Mapunjo na Mfamasia kutoka Wizara hiyo, Mercy Masuki.
Taarifa ikitolewa...
Baadhi ya Wafanyakazi wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo.
Wanahabari wakiwa kwenye mkutano huo
Picha ya pamoja...
Na Dotto Mwaibale
WAZIRI wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Ummy Mwalimu amesema bei za dawa,
vifaa tiba na Vitendanishi vya maabara zinazonunuliwa na kusambazwa Boahari ya
Dawa (MSD) zimepungua bei kwa asilimia 15 hadi 80 ukulinganisha na mwaka jana
kutokana na hatua ya MSD kuanza utaratibu wa kununua moja kwa moja kutoka kwa
wazalishaji, kama alivyoagiza Rais Dk.John Magufuli.
Waziri huyo ameyasema hayo kwenye mkutano wake na
waandishi wa habari, alioufanya ofisi za Makao Makuu ya Bohari ya Dawa MSD,
Keko, Dar es Salaam leo huku akizielekeza Halmashauri, Hospitali na Vituo vya Afya kutumia bei
elekezi ya dawa iliyotolewa ma Wizara ya Afya ambayo ipo kwenye kitabu cha
orodha ya bei cha MSD.
MSD kwa sasa
inaagiza dawa moja kwa moja kutoka kwa wazalishaji wa nchi zipatazo 20 ambazo ni pamoja na
Kenya, Uganda, Afrika Kusini, India, Bangladesh, Pakistan, Jamuhuri ya Watu wa
Korea, China, Ujerumani, Uingereza, Uswisi, Denmark, Ufaransa, Ubelgiji,
Italia, Romania, Marekani, Cyprus, Falme za Kiarabu, na Tanzania.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa MSD Bwana Laurean
Bwanakunu amesema tayari wametoa mikataba 73 kwa wazalishaji ambapo kati ya
hiyo 46 ni ya wazalishaji wa dawa ambao wanatoka nchi za Uganda, Denmark,
Ufaransa, Ujerumani, China, Afrika Kusini, Nchi za Falme za Kiarabu, Bangladesh,
India, Kenya na Tanzania ambao wanazalishia aina 178 za dawa.
Baadhi ya dawa hizo ni pamoja na dawa ya chanjo ya homa
ya ini (hepatitis B Vaccine) awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 22,000 sasa inauzwa
shilingi 5,300, Dawa ya sindano ya Diclofenac kwa ajili ya maumivu (vichupa 10)
awali ilikuwa ikiuzwa shilingi 2,000 sasa inauzwa shilingi 800 na Dawa ya
kupambana na maambukizi ya bakteria (Amoxicillin/Clavulanic Acid Potassium
625mg) yenye Vidonge 15 awali iliuzwa shilingi 9,800 sasa inauzwa shilingi
4,000.
Kwa upande wa vifaa tiba amesema jumla ya wazalishaji 18
wamepata mikataba ambao wanatoka Uingereza, Ujerumani, India, Kenya na
Tanzania, kwa ajili ya aina 195 za vifaa tiba. Aidha, kwa upande wa
vitendanishi vya maabara, jumla ya wazalishaji 9 kutoka nchi za Uingereza,
Ujerumani, Ubelgiji, Romania, China, India na Kenya wamepata mikataba kwa ajili
ya aina 178 za vitendanishi vya maabara.
Kwa mujibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto, Serikali ya awamu ya tano imeboresha kwa kiasi kikubwa
hali ya upatikanaji wa dawa nchini ambapo bajeti ya dawa, vifaa tiba,
vitendanishi vya maabara na chanjo kwa mwaka huu wa fedha 2017/2018 ni shilingi
Bilioni 269 kutoka Bilioni 251 ya mwaka jana wa fedha wa 2016/2017.
0 comments:
Post a Comment