Mwanajeshi wa Misri |
Zaidi ya askari ishirini wa Misri wameuawa na kujeruhiwa
katika mashambulizi yaliyofanywa kwenye vizuizi viwili vya usalama katika eneo
la Rasi ya Sinai.
Kwa mujibu wa duru za kiusalama nchini humo,
washambuliaji hao waliyalipua magari yao yalikuwa na vilipuzi wakati
walipokaribia kwenye vizuizi hivyo katika mji wa mpakani wa Rafah kaskazini mwa
Sinai.
Wakati huo huo, jeshi la nchi hiyo limesema kuwa askari
26, akiwemo mmoja mwenye cheo cha kanali, waliuawa au kujeruhiwa katika
mashambulizi hayo mawili, bila kutoa idadi kamili.
Hata hivyo, mashirika ya habari yamelezea idadi ya
waliokufa kuwa ni 10, kwa mujibu wa duru mbalimbali.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Associated Press,
shambulizi moja lilifuatiwa na milio ya risasi kutoka kwa wanamgambo
waliofunika nyuso zao ambao walikuwa wakitembea.
Jeshi la Misri limesema kuwa vikosi vyake vimewaua
wanamgambo wasiopungua 40 na kuharibu magari yao 6 katika operesheni
iliyofuatia mashambulizi hayo.
Hakuna kundi lililodai kuhusika na mashambulizi hayo ya
huko Sinai ambayo ni ngome ya kundi moja lenye mafungamano na kundi la Dola la
Kiislamu (Daesh).
Mashambulizi ya wanamgambo yameua mamia ya wanajeshi na
polisi katika eneo hilo la jangwa kubwa tangu mwaka 2013. Hivi karibuni tu,
chanzo kimoja cha usalama kilisema kuwa Daesh walitega bomu huko Sinai lililoua
polisi watatu.
Kundi lenye mafungamano na Daesh lijulikanalo kama Wilayat
Sinai, limekuwa pia likiwashashambulia Wakristo wa jamii ya Wakhufiti (Coptic).
Zaidi ya Wakhufiti 100 wameshauawa katika mashambulizi hayo tangu Desemba mwaka
jana.
Siku ya Jumanne bunge la nchi hiyo liliridhia uamuzi wa
Rais Abdel Fattah el-Sisi wa kuongeza hali ya dharura nchini kote kwa muda wa miezi
mitatu zaidi katika juhudi za kukabiliana na ugaidi katika eneo la Sinai.
0 comments:
Post a Comment