AJALI YA TRENI YASABABISHA MAAFA MAKUBWA NCHINI HISPANIA



Idadi ya vifo katika ajali ya treni iliyoanguka jana kaskazini mashariki mwa Hispania imepanda mpaka kufikia watu 77, huku zaidi ya watu 140 wakiwa wamejeruhiwa.


Ajali hiyo mbaya ilitokea jana Jumanne baada ya treni kuacha njia takribani kilometa tatu kutoka stesheni ya Santiago de Compostela katika mkoa wa kaskazini magharibi wa Galicia. 

Treni hiyo ilikuwa ikisafirisha abiria 218 na wafanyakazi 4 kutoka mjini Madrid kwenda mji wa Ferrol ambao ni maarufu kwa shughuli za ujenzi wa meli kwenye mkoa wa pwani wa Galicia.



Msemaji wa mahakama kuu ya Galicia amesema kuwa miili ya watu 73 imetolewa kutoka kwenye eno hilo na waathirika wanne walipoteza maisha yao wakiwa hospitali. Jumla ya watu 143 walipata majeraha mbalimbali.  


Vyombo vya habari vinasema kuwa treni hiyo iliacha njia kutokana na mwendo kasi.


Hata hivyo, msemaji wa shirika la reli la serikali, Renfe, alisema kuwa ni mapema mno kusema chochote kuhusu chanzo cha ajali. 


“Kuna uchunguzi unafanyika na tunapaswa kusubiri. Muda si mrefu tutajua kuhusu kasi husika pindi tutakapokichughuza kikasha cheusi," alisema Renfe.


Naye kiongozi wa serikali ya mkoa, Alberto Nunez Feijoo, alisema, "Kuna miili imelala kwenye reli. Hii ni hali ya kusikitisha sana.” 


Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu wa Hispania, Mariano Rajoy, ambaye ni mzawa wa mkoa wa Santiago de Compostela, ametembelea eneo la tukio.


Msiba huu unachukuliwa kuwa miongoni mwa majanga makubwa kabisa katika historia ya usafari wa reli nchini Hispania. 

Mwaka 1972, tereni ilianguka mjini Andalusia na watu  77 wakapoteza maisha. 
Share on Google Plus

About mahamoud

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.

0 comments:

Post a Comment