Mario Balotelli amekiri kuwa anafikiria siku moja kurudi
kwenye Ligi Kuu ya Uingereza… lakini sio katika klabu yake ya zamani ya Liverpool.
Mshambuliaji huyo wa Italia – ambaye sasa hivi
anafurahia kufanya vizuri katika klabu yake ya Nice ya Ufaransa – aliwaelezea Liverpool
kuwa ni timu “nzuri” lakini akatupilia mbali uwezekano wa kurudi kwenye timu
hiyo.
Wakati akieleza kuwa pendeleo lake la kwanza nchini
Uingereza ni Manchester City, hakuficha pia upendo wake kwa Arsenal.
"Nikirudi Uingereza bila shaka sitaenda Liverpool,"
Balotelli aliliambia shirika la habari la Uchina, Xinhua.
"Kwa sababu nilijikuta nikifanya vibaya sana
nilipokuwa Liverpool. Timu ilikuwa nzuri na mashabiki walikuwa wazuri sana,
lakini kamwe siwezi kurudi Liverpool.
"Timu ya kwanza kabisa ninayoiwazia huko Uingereza
ni Manchester City, na nyingine ambayo nimekuwa na mapenzi nayo ni Arsenal. Haimaanishi
kuwa nitaenda kucheza huko. Ninazipenda tu.”
0 comments:
Post a Comment