Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.4 kwenye kipimo cha Richter
limetokea katika JImbo la Aceh nchini Indonesea mapema leoJumatano na kuua watu
wasiopungua 25, kumjeruhi mtu mmoja na kusababisha makumi ya nyumba kuanguka,
maafisa wa serikali wamesema.
Tetetmeko hilo limetokea saa 11 alfajiri kwa majira ya
eneo hilo ambapo kitovu chake kilikuwa kilometa 18 kaskazini mashariki mwa
wilaya ya Pidie Jaya, kwenye kina cha kilometa 10, mamlaka ya kitaifa ya
jiolojia imesema.
Hata hivyo, hakuna tahadhari ya tsunami iliyotolewa.
Mkuu wa idara ya majanga katika walaya ya Pidie Jaya
katika jimbo la Aceh, amesema kuwa watoto 8 ni miongoni mwa waathiria wa
tetemeko hilo.
"Idadi ya vifo inaweza kuongezeka kwa sababu
taarifa zinaendelea kutufikia kutoka wilaya mbalimbali,” Puteh Manaf amenukuliwa
na mtandao wa acehkita.com saa 6 baada ya tetemeko hilo.
Kufuatia tetemeko hilo, watu walihamanika wakayakimbia
majumba yao huku tetemeko kubwa likisikika katika eneo lote la Pidie Jaya.
"Kwa mujibu wa taarifa mpya kutoka idara ya majanga
ya eneo hilo, kuna majengo kadhaa ambayo yameanguka," Nugroho amesema.
Indonesia iko ndani ya eneo la Bahari ya Pacific
lijulikanalo kama “Ulingo wa Moto”, ambalo hutokewa na matetemeko mengi.
Mwezi Juni, tetemeko lenye ukubwa wa 6.5 liliharibu
majengo katika Kisiwa cha Sumatra magharibi mwa nchi hiyo, huku tetemeko hilo
likisikika katika maeneo ya nchi za Singapore upande wa kaskazini wa Malaysia.
Mnamo Desemba 26, 2004, tetemeko lenye ukubwa wa 9.1 lilipiga
katika eneo la pwani ya mashariki ya Sumatra likasababisha tsunami iliyoua watu
wapatao 230,000 na kutandaa katika pwani za Sri Lanka, India, Malaysia,
Indonesia na Thailand.
0 comments:
Post a Comment