Samuel Eto’o alipomuoa Georgette Tra Lou |
Nyota wa klabu ya Antalyaspor ya nchini Uturuki, Samuel
Eto’o, anakabiliwa na kifungo kisichopungua miaka 10 jela na kitita cha faini
kipatacho €14m kwa makosa ya ukwepaji wa kodi aliyoyafanya alipokuwa akicheza
soka nchini Hispania.
Kwa mujibu wa gazeti la El Pais la nchini Hispania,
mkongwe huyo raia wa Cameroon alifanya makosa hayo kuanzia mwaka 2006 mpaka
2009 alipokuwa akichezea klabu ya Barcelona, na aliweza kukwepa kulipa kodi ya
euro milioni 3.5 kupitia mfumo haramu wa haki zake za matangazo uliotengenezwa
kiustadi.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Eto’o mwenye umri wa miaka 35,
alianzisha makampuni mawili, moja nchini Hispania iitwayo Bulte aliyoifungua
mwaka 2002 na nyingine nchini Hungary iitwayo Tradesport ambayo yalimuwezesha kuhamisha
kijanja haki zake za matangazo na kukwepa kulipa kodi. Pia kupitia muundo wa
kampuni hiyo, anatuhumiwa kukwepa kulipa kodi kwa kiasi kikubwa cha pesa (karibu
euro milioni 1.5 na 3 kwa msimu) alichokipokea kutokana na udhamini wa kampuni
kubwa ya vifaa vya michezo ya Puma.
Waendesha mashitaka wa Hispania wanataka Eto’o apigwe
faini ya karibu £12m (€14m).
Source: http://ameyawdebrah.com/
Kupata habari na taarifa mbalimbali kupitia WhatsApp:
+255 712 566 595
0 comments:
Post a Comment