Kwa kiasi fulani mwanamke ni kiumbe mgumu kumuelewa, na
linalomfanya awe hivyo ni kwamba wanawake wote wanatofautiana. Ili mwanaume
apate kumuelewa, wakati fulani huenda kuchukua ushauri kwa marafiki, lakini
wakati fulani mawazo yao huwa sahihi au huwa sio sahihi.
1. Mwanamke
anapenda ahisi kuwa yeye ni wa kipekee. Anapenda ahisi kuwa mumewe anamuwaza na
anapenda kumjali. Na hilo sio gumu hata kidogo. Ujumbe mfupi wa simu
utakaomtumia ukiwa kazini, kujali hisia zake anapokuwa na huzuni na busu laini
unapotoka kazini vinatosha kumuonesha
yote hayo.
2. Mke
anapenda mume amsikilize na aheshimu mawazo yake. Mume anapomsikiliza mkewe huimarisha
sana mafungamano yao. Mke hataki ukubali kila anachosema, bali anataka
usikilize kila analosema, iwe ni wazo, kisa au malalamiko.
3. Siku
zote mwanamke anapenda kusikia ukweli kutoka kwa mumewe. Anapohisi kuwa mumewe
hamwambii ukweli huanza kuwa na shaka nyingi na inakuwa ngumu kumshawishi tena.
Unatakiwa kuwa muwazi kama unampenda mkeo na unataka utulivu na upendo.
4. Kusaidia
kazi za nyumbani au kuangalia watoto. Siku zote mwanamke anahitaji usaidizi.
Tafiti mbalimbali zimesisitiza kuwa wanaume wanaowasaidia wake zao nyumbani na
kutunza watoto hupata mahabba motomoto kama zawadi kutoka kwa wake zao, kwa
sababu usaidizi huo humpa nguvu mwanamke na kumfanya amheshimu mumewe na
kumthamini.
5. Mwanamke
ni kiumbe mwenye hisia kali sana kwenye ukosoaji. Kumuelewa mwanamke inahitaji
kutengeneza njia za kuzungumzia malalamiko zisizoathiri hisia zake hata kidogo.
6. Akili
ya mwanamke inahitaji muda mrefu zaidi ili kufuta athari za ugomvi uliopita.
Mwanamke hasahau dhulma aliyofanyiwa au ugomvi kwa urahisi. Anahitaji muda
mrefu zaidi ya ule anaouhitaji mwanaume.
7. Mwanamke
anampenda mwanaume anayeweka wazi mambo ya maisha yake. Mwanamke anapenda ajue
kila kitu kuhusu mumewe, sio kwa lengo la kumdhibiti au kumkosoa, bali anataka
ahisi kuwa mafungamano yake kwa mumewe ni makubwa.
8. Mwanamke
hapendi mwanaume awe mtu wa kumpa amri. Utafiti unasema kuwa mwanamke anapenda
awe na uhuru wa mawazo na uchaguzi, anapenda ahisi kuwa mumewe anamuunga mkono
bila kumpa amri.
9. Linapotokea
tatizo au kutoelewana, mwanamke anapenda lizungumzwe, hilo humfanya ahisi kuwa
yu karibu zaidi na mumewe. Hata hivyo, jambo hilo linapingana na tabia ya
wanaume ambao wanapendelea kumaliza jambo haraka au kwa kulifukia.
10. Mwanamke
anapenda mumewe amtazame pindi anapozungumza. Mwanamke anadhani kuwa mume
anapokuwa hamtazami anakuwa hamsikii. Hili linaweza kuwa jambo la ajabu kwako,
lakini ndio ukweli.
Kwa hisani ya: www.ndoamaridhawa.com
0 comments:
Post a Comment