Askari wa Pakistan wakiwa wameuzingira mtaa unaoelekea
kwenye eneo palipotokea shambulizi la bomu kwenye viunga vya mji wa Peshawar Septemba
2, 2016.
|
Kwa uchache watu 10 wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka nje ya mahakama moja ya wilaya katika jimbo la Khyber Pakhtunkhwa kaskazini magharibi mwa Pakistan, vyombo vya habari vimeripoti.
“Kwanza kulikuwa na mlipuko mdogo uliofuatiwa na mlipuko
mkubwa” leo asubuhi nje ya mahakama iliyopo kwenye kitongoji cha Wakristo
karibu na Bwawa la Warsak katika mkoa wa Khyber, kilometa 20 (maili 12) kaskazini
magharibi mwa Mji wa Peshawar, afisa wa uokoaji katika eneo hilo, Haris Habib,
amesema.
Muda mfupi baadaye, kundi la wanamgambo la Jamaat-ul-Ahrar
lenye mafungamano na kundi la Taliban la nchini Pakistan lilidai kuhusika na
shambulizi hilo.
Msemaji wa Taliban, Ehsanullah Ehsan, amesema kuwa kulikuwa na “vifo
kadhaa” katika shambulizi hilo.
(Habari itaendelea........)
0 comments:
Post a Comment