Tume ya haki za Binadamu na Utawala bora imelitaka Jeshi
la polisi nchini na Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kuacha kutumia
lugha zenye viashiria vya uvunjifu wa amani na ukiukwaji wa haki za binadamu
badala yake zifanye majadiliano yatakayoleta suluhisho kuhusiana na katazo la
maandamano na mikutano ya siasa nchini.
Tume ya haki za binadamu na utawala bora imefikia uamuzi
huo katika mkutano maalum uliotishwa
jijini Dar es salaa na kuwahusisha viongozi mbalimbali akiwemo Msajili
wa Vyama Siasa nchini Jaji Francis Mtungi, Katibu mkuu wa Chadema Vincent
Mashinji, ingawa waalikwa wengine akiwamo mkuu wa jeshi la polisi, mwanasheria
mkuu na chama cha mapinduzi ambao nao kwa mujibu wa tume hiyo walipata mwaliko
lakini hawakuhudhiria, huku ikielezwa kuwa IGP na mwanasheria mkuu walitoa
hudhuru.
Mwenyekiti wa tume hiyo Bahame Nyanduga amesema nia ya
mkutano huo ni kupata suluhu ya kudumu kuhusiana na agizo la lilitolewa na
jeshi la polisi June 7 mwaka huu kuhusu kupiga marufuku maandamano na mikutano
ya siasa huku CHADEMA ikitangaza kufanya hivyo nchi nzima ifikapo september 1
mwaka huu kupitia operation UKUTA.
Aidha kuhusiana na operesheni “UKUTA” Bw. Nyanduga
amekitaka chama hicho kuachana na Neno UDIKTETA kwa kuwa Tanzania ni nchi
inayoongozwa kwa misingi demokerasia.
Pia Mwenyekiti Nyanduga ameishauri CHADEMA kuachana na
operesheni waliyoita upingaji wa Udikteta Tanzania badala yake wasubiri Tafsiri
sahihi itakayotolewa na mahakama kufuatia kufungua shauri hilo katika mahakama
kuu kanda ya Dar salaam pamoja na lile la Kanda ya Mwanza.
CHANZO: Channel Ten
0 comments:
Post a Comment