
Watu wawili wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi kwenye
kituo kimoja cha afya mjini Florida nchini Marekani.
Kwa mujibu wa maafisa wa eneo hilo, tukio hilo limetokea
leo saa 8 usiku kwa majira ya nchi hiyo kwenye ghorofa ya tatu ya kituo cha Parrish
Medical Center in Titusville.
Mtu aliyekuwa na bunduki alimpiga risasi bibi kizee
mmoja aliyekuwa mgonjwa na mhudumu mmoja wa hospitali hiyo.
Polisi wanasema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa, lakini
sababu ya kufanya tukio hilo haijajulikana.
Kwa mujibu wa kituo cha Marekani cha Kudhibiti na Kuzuia
Magonjwa (CDC), bunduki husababisha vifo vya zaidi ya watu 33,000 nchini humo
kila mwaka, idadi ambayo inajumuisha, ajali, mauaji na kujinyonga.
Takwimu zinaonesha kuwa nchini humo kuna kiasi cha
bunduki milioni 270 mpaka 300, ambayo ni karibu bunduki moja kwa kila mtu.
(Kupata habari kupitia WhatsApp, ungana nasi kwa: +255 712 566 595)
0 comments:
Post a Comment